Mzimuni

Monday, October 14, 2013

NATUMIA GHARAMA KUBWA KUANDAA FILAMU ZANGU-JIMMY MASTER


Jimmy Mponda
Jimmy Master mtayarishaji wa filamu Swahilihood.
MUASISI wa filamu msanii Mahiri katika filamu za mapigano Tanzania Jimmy Mponda ‘Jimmy Master’ anasema kuwa moja ya sifa au ubora wa kazi zake kudumu kwa muda mrefu ni kutokana na umakini, ubora na matumizi ya gharama katika uaandaaji wa filamu zake hatumii muda mfupi kutayarisha filamu.

.
Jimmy mponda
Jimmy Master akiwa katika pozi la mazoezi ya kimapigano
Jimmy Mponda 560
Jimmy Mponda 566 

“Filamu zangu zinatumia gharama kubwa katika kuandaa lakini kitu kingine ni muda wa kutosha kwani toka niingie katika uandaaji wa filamu sijawahi chini ya miezi sita na kuendelea, sinema za mapigano ni ngumu lazima ujue martial arts somo ambalo mimi ni mwalimu,”anasema Jimmy Master.
Jimmy ndiyo muasisi wa filamu za Kibiashara sinema nchini yake ya kwanza Shamba kubwa alirekodi mwaka 1995 akishirikiana na Kaini Jijini Tanga, filamu nyingine ni Kifo Haramu, Misukosuko, Double J, na filamu nyingi na sinema za Jimmy ni tofauti sana na nyingine zinatoka kwa matoleo zaidi ya nne kama ilivyo Double J 1,2,3,4 na 5 Final.Maelezo ya stori hii yanatoka katika gazeti moja , nilipokuwa nikihojiwa na
chombo hicho sikuchache zilizopita.

Tuesday, September 10, 2013

DOUBLE J FINAL




 
 
 FILAMU   ya Double J Final ni kazi ambayo imepokelewa na wapenzi wa filamu Bongo na kuamini kuwa ni kazi ya mwaka, nimekuwa  niakitumia muda mwingi katika utayarishaji wa kazi zangu  ambazo zimekuwa bora kila zitokapo.
.
Double J
Filamu ya Double J


Jimmy Master
Jimmy Master nikiwa katika  action.

Wednesday, August 21, 2013

Soma heka heka za ujio wa J Plus katika filamu ya Doble J Final



MSANII nguli katika anga za tasnia ya filamu nchini Jimmy Mponda
a.k.a  Jimmy Master baada ya  mashabiki wake kuwa wanamuuliza
kuhusu muendelezo wa sinema ya Double J iliyotoka katika
mfurulizo wa kwanza na wapili jamaa amefunguka kuwa
kutua na ujio wa Doble J Final.

Nyota huyo ambaye sinema zake zimeonekana kuwa na mapigano ya
kutisha amefunguka kuwa kama kawaida yake yamo matukio yanayoambatana
na matukio sahihi ya kipelelezi yanayovutia wadau kupatwa na hisia mara tu
watakapoiona filamu hiyo.


"Wadau wengi walikuwa wakiniuliza muendelezo wa sinema hii,
napenda kuwatangazia kuwa siku si nyingi wataanza
kuipata sinema hii,"alifunguka J Plus.

Ndani ya ujio huo jamaa amemshirikisha mbambe mwingine wa filamu
za mapigano Ibrahim Mbwana 'Bad Boy' pamoja na nyota kadhaa
kama Charles Magari pamoja na Hashim Kambi na Veronica Viankero.

Msome J Plus akifunguka mambo kedekede!

Image
NIKIWA  ndiye nyota wa filamu za ‘Misuko Suko’ ambayo ilionekana kuwa na mguzo   na kuteka mashabiki lukuki  hali iliyosababisha itolewe kuanzia toleo la
kwanza hadi la tatu kwa kipindi cha nyakati tofau.
Kupitia filamu hizo ambazo zinaubabe mwingi ndani ya filamu hizo  kuna mijeba yenye maumbile ya ‘Inglish-Body’ na kuna heka heka za kibabe ambazo
zimeijengea filamu ya ‘Misuko Suko’umaarufu mkubwa.
Mtayalishaji wa filamu hizo nimimi mwenyewe Jimmy Mponda ‘Jimmy Master’ ambapo natiririka katika makala hii.
Nilianza sanaa kwa kujihusisha na mchezo wa sarakasi , mwaka 1978 hadi
kufikia mwaka 1980 nilijiunga na kikundi cha Yusta ambacho kilijihusisha na Sarakasi ngoma na maigizo ya Stejini.
Mwaka 1986 nilianza kujihusisha na biashara na wakati huo huonikaanza pia kujihusisha na mchezo wa mapigano na Sarakasi nkiwa mkoani Arusha (YMCA).
Kwa kuwa elimu ni kama nguzo ya kumuongoza mwanadamu kumudu mazingira yanayomzunguka Mponda ni alisoma shule ya msingi na sekondari Arusha amabpo mwaka 1986 ndio mwakaniliomaliza
kidato cha nne mkoani  Arusha.
Mwaka 1999 nilikuja Dar , na mtazamo wangu niliuhamishia Dar  mwaka 1989 hadi 1990 mwishoni.
Nikiwa  jijini Dar nilikuwa nikifanya biashara ya kupeleka bidhaa mbali mbali
mikoani.
Mwishoni mwa mwaka 1990 , niliamia mkoni Taanga ambapo nilifanya biashara na mazoezi.
Nikiwa  katika pilika pilika za kibiashara nilikutana na wenzake wengine na kuanzisha kundi lililoitwa (Black Ninja Group), ambapotulianza  kujihusisha na
uandaaji wa shoo za mapigano.
Tulianza  kuipenyeza sanaa yetu  hiyo kwa kuvuka mipaka ya nchi za Kenya na Uganda ikiwa ni   mwaka 1992 hadi 1993.
Ambapo mwaka 1994 tulipata wazo la kufanya filamu, tulitafuta mtunzi wa kuchukua matukio ya video na kuandaa fialmu ya ‘Shamba Kubwa’.
Filamu hiyo baada ya kukamilika tuliweza kufanya uzinduzi kwenye mikoa ya Tanga , Mwanza na Iringa.
Kuanzia hapo Jimmy Master nilibakiza asilimia 60 katika kufanya masuala ya filamu na asilimia 40 nikazibakisha kwenye mawazo ya biashara.
''Filamu iliyofuata ilikuwa ikiitwa ‘Unga Adui wa Haki’ ilizungumzia
madawa ya kulenya.
“Ilikuwa mwaka 1996 ambapo mwaka uliofuata nilirudi tena jijini Dar es Salaam , nikitokea Tanga ambapo ndipo nikawa nimehamia jijini hapa moja kwa moja,”alisema Jimmy Master.
Mwaka 200 niliandaa filamu iliyoitwa ‘USIA’ ambapo akujivika huusika wowote licha ya yeye kuwa
muhusika.
Hapo nilifanikiwa kuibua vipaji mbali mbalivya Wasanii katika muziki wa Bongofleva .
Licha ya kujipatia umaarufu awali kwenye filamu ya ‘Shamba kubwa’ filamu ya ‘Misuko Suko’ iliyotoka mpaka matoleo
matatu ndio iliyokuza zaidi umaarufu na mafaniko yake mengi katika tasnia
hiyo ya filamu.
“Kunamafaniko lukuki amabyo ninayaona kwa sasa baada ya kutoa matoleo hayo ,
ambapo niliweza kupata ‘Ma-msapu’ na kufunga ndoa .
“Kwa sasa mie ni baba wa watoto wawili, na pia nimeongezea kuwa mjasiliamali, namiliki duka   linalojihusisha na huuzaji wa filamu karia koo likiuza
filamu mbali mbali na vifaa vya video Production namengineyo.”
Pia  kwa sasa tayari nimeingiza sokomi filamu mpya iitwayo ‘Doble J’ikiwa   imeandaliwa na kampuni  yangu
iitwayo ‘Jimpowood Campani LTD ,inayo patikana maeneo ya DDC Magomeni jijini
Dar es Salaam.
 mafanikio mengine niliyoyapata kwa hivi sasa kwenye tasnia hii ya filamu ni kumiliki gari ainaya
Toyota Mark 11 lenye thamani ya milioni
16.
 Pia baadhi ya matukio ambayo sirahisi kuyasahau maishani mwangu ni lishafiwa na mama  mzazi , ambapo katika maisha
ambayo ni  nguzo duniani
“Mama alifariki dunia nikiwa bado naitaji nasaha zake lakini mungu alimpenda zaidi.”
 nakumbuka zaidi tukio lililowahi kunitokea  la kupatwa na ajari mbaya ya gari maeneo ya Bia ramuro mkoani Kagera mwaka  1998 ambapo gari lilipinduka zaidi ya mara nne lakini mungu alisaidia nikatoka salama.